Ijumaa 11 Septemba 2026 - 16:01
Rais wa Baraza la Itikadi ya Kiislamu la Pakistan Akutana na Ayatullah al-Udhma Hafiz Bashir Najafi Katika Ziara Yake huko Najaf Ashraf

Hawzah/ Mufti Raghīb Hussein Na‘īmī, Mwenyekiti wa Baraza la Itikadi ya Kiislamu la Pakistan, amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah al-Uzma Hafiz Bashir Hussein Najafi huko Najaf Ashraf.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Mufti Raghīb Hussein Na‘īmī, Mwenyekiti wa Baraza la Itikadi ya Kiislamu la Pakistan, amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah al-Udhma Hafiz Bashir Hussein Najafi huko Najaf Ashraf.

Katika kikao hicho, mada mbalimbali zikiwemo umoja na mshikamano wa Umma wa Kiislamu, mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as), kueneza maadili ya kidini na Kiislamu, pamoja na njia za kuimarisha undugu miongoni mwa Waislamu, zilijadiliwa na wakabadilishana mawazo kuhusu masuala hayo.

Ayatullah al-Udhma Hafiz Bashir Hussein Najafi, katika kikao hicho, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa Waislamu na Qur’ani Tukufu pamoja na mafundisho ya Ahlul-Bayt (as), alisema: Umma wa Kiislamu unapaswa kujenga maisha yake ya mtu binafsi na ya kijamii kwa misingi ya mafundisho ya Qur’ani Tukufu na mwenendo wa Ahlul-Bayt (as); kwa sababu kuwapenda Ahlul-Bayt (as) na kufuata mwenendo wao ni sehemu muhimu ya mafundisho halisi ya Kiislamu.

Aidha, akizungumzia umuhimu wa kuimarisha umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu, alisisitiza ulazima wa kuimarisha moyo wa undugu miongoni mwa Waislamu na kulinda maadili ya kidini na Kiislamu.

Ayatullah al-dhzma Bashir Najafi aliendelea kuwataka Waislamu kumpenda Mtume Mtukufu (saww) na familia yake tukufu kuwa mhimili na mwongozo mkuu wa maisha yao, akasema: Mtume Mtukufu (saww) mwenyewe alikuwa na mapenzi makubwa kwa Ahlul-Bayt (as), na alikuwa akiusia na kuusisitizia Umma wa Kiislamu kuwasiliana na familia yake tukufu, kuwapenda na kushikamana nao.

Katika kuendelea kwa mkutano huo, Mufti Raghīb Hussein Na‘īmī alimshukuru Ayatullah al-Udhma Bashir Najafi kwa kumpatia muda wake na kumpokea kwa ukarimu, na akatoa pongezi na heshima kwa huduma zake za kidini, kielimu na kijamii.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha